Kwa
upande mmoja benki ya kiislamu inajiendesha kwa bidhaa za Amana ambazo benki
huweza kukusanya fedha kutoka kwa wateja wake ambao wana akiba.
Benki
kama chombo cha kati cha kuwaunganisha waeka akiba na wawekezaji inatengeneza
bidhaa za kibenki ambazo zitaiwezesha kukusanya fedha kutoka kwa wateja wake.
Bidhaa
hizo hutofautiana kwa sifa mbalimbali kutokana na aina ya mikataba ya kisha’ria
inayotumika kuunda bidhaa hizo.
Moja
ya bidhaa ambayo benki hutumia kukusanya fedha kwa wateja wake ni akauti ya hundi.
Kama
ilivyo kwenye benki zisizo za kiislamu akaunti hii hutumika kuhifadhi fedha za
wateja kwa usalama.
Huduma
hii ya kutunza fedha kwa usalama hutolewa bure bila malipo yoyote.
Katika
akaunti hii mteja anaruhusiwa kuchukua fedha zake wakati wowote. Ili kurahisisha
utowaji wa fedha benki kwa wateja, benki hutoa huduma mbalimbali kama kadi ya
kutolea fedha (ATM card), hundi, hundi ya msafiri, huduma za kibenki kwa simu
na kadhalika.
Akaunti
hii huundwa kwa kutumia mkataba (Akd) wa Al-Wadiah au Qardh hasan.
Akauti
ya hundi inayoundwa kwa mkataba wa Al- Wadia mara nyingi huitwa Akaunti ya
Al-Wadiah.
Al-Wadiah
ni mkataba (Akd) baina ya wenye kutaka kuhifadhiwa fedha (mteja) na wenye
kuhifadhi fedha (Benki) kwa madhumuni ya mteja kuhifadhi fedha zake kwa usalama
zaidi.
Katika
mkataba huu Benki ya Kiislamu kwa upande mmoja inakubali kuchukua dhamana kwa
mteja juu ya kumtunzia fedha zake na itazirejesha fedha wakati wowote
anapozihitaji, ima zote kwa pamoja au sehemu ya fedha hizo. Pia inakubali kuzitumia
fedha za mteja katika biashara au kuwekeza fedha za mteja katika biashara iliyo
halali katika misingi ya Shariah ya Kiislamu kwa lengo la kupata faida.
Mteja
alieweka fedha katika Benki ya Kiislamu kwa upande wa pili anakubali fedha
aliyoweka kutumiwa na Benki katika biashara iliyohalali katika misingi ya
Shariah ya Kiislamu.
Faida
itakayopatina katika biashara hiyo hapaswi kupewa wala kudai. Ila Benki ikiamua
inaweza kumpatia gawio kwa njia ya zawadi (hibah).
Kwa
upande mwingine pale benki itakapo tumia mkataba wa Qardh hasan katika akaunti hii mteja atahesabika kaikopesha
benki fedha hizo bila riba kwani mkataba huu ni wa mkopo usio na riba.
Benki
itatumia fedha hizo katika miradi yake bila kumpa faida yoyote mteja wake kwani
faida hiyo itahesabika kama riba. Mteja atachukuwa fedha zake wakati wowote
anapohitaji.
Walengwa
wa akaunti hii ni wale wote wanaohitaji kuweka fedha zao mahali salama ambapo
fedha zao zitatumika kwa kuzingatia shari’ah ya kiislamu.
Wateja
hao ni watu wote Waislamu na wasiokua waislamu wenye umri usiopungua miaka 18,
Wafanyabiashara, Wakulima, Wafanyakazi,Serikali
na Idara zake, Mashirika ya Serikali, Makampuni ya watu binafsi, Mashirika na Taasisi zisizo
za Kiserikali, Watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane (18) wanaruhusiwa
kufungua Akaunti chini ya udhamini wa mzazi au mlezi.
No comments:
Post a Comment