Shukrani
njema anastahiki Mola wa walimwengu wote. Rehma na Amani zimfikie Mtume aliye
rahma kwa walimwengu wote. Kisha maamkizi mema kwa wenye kufuata muongozo.
Benki
ya kiislamu ni benki inayofuata shari’ah ya kiislamu kikamilifu katika miamala
inayofanya na katika shughuli zake zote kwa ujumla.
Ili
kudhibiti shughuli za kibenki kwenda katika taratibu za kiislamu ni lazima
katika muundo wa benki inayotoa huduma za kibenki kwa kufuata utaratibu wa
kiislamu kuwa na bodi ya kusimamia Shari’a. Kwa ujumla bodi hii inamajukumu
yafuatayo:
Moja,
Kutoa fatwa juu ya bidhaa na miamala ya kibenki. Kila bidhaa mpya ya benki ni
lazima iidhinishwe na bodi hii kuwa imekidhi masharti, kiwango na kukubalika
kishari’ah.
Mbili,
Kufanya ukaguzi wa Shari’ah kuhakikisha bidhaa na miamala kwa ujumla inafuata
Sharia’h kikamilifu.
Tatu,
Kuondoa mapato au faida iliyopatikana kwa kukiuka misingi ya Uislamu.
Nne,
Kuishauri benki juu ya uugawaji wa faida/pato kwa wamiliki wa benki au kwa
waeka akiba (wateja wa benki).
Tano,
Kukokotoa malipo ya Zaka.
Sita,
Kutoa muongozo kwa benki juu ya mambo yanayohusisha Shari’ah ya kiislamu na
jukumu la benki kwa jamii kwa ujumla.
Hayo
ni baadi ya majukumu ya bodi hiyo, ingawa kwa ujumla majukumu ya bodi hii
yanatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine.
Pia
kuna aina aina tatu za bodi ya kusimamia shari’ah.
Aina
ya kwanza ni bodi ya Shariah ya kimataifa, mfano wa bodi kama hii ni AAOFI
ambayo jukumu lake kuu ni kuandaa na kuchapisha kanuni na miongozo
inayozingatia Shari’ah ili kuoanisha utekelezaji wa miamala ya kifedha kwa
kufuata utaratibu wa kiislamu duniani.
Aina
ya pili ni bodi ya Shari’ah ya kitaifa, bodi hii ina mamlaka katika nchi
kusimamia na kutunga sera juu ya usimamizi wa utekelezaji wa Shari’ah. Bodi hii
ndio ina mamlaka ya mwisho ya kusimamia taasisi za kifedha juu ya utekelezaji
wa Sharia’h katika ngazi ya nnchi. Bodi kama hii zipo Malaysia, Pakistan,
Sudan, Indonesia.
Aina
ya tatu ni bodi ya kusimamia Shari’ah katika ngazi ya Taasisi, bodi hii inafanya
kazi katika ngazi ya Taasisi husika tu na kila benki inayotoa huduma kwa
utaratibu wa Uislamu ina bodi yake yenyewe. Utaratibu huu hutumika hapa nchini
Tanzania.
Swali
maarufu kwa watu wengi ni vipi benki ya kiislamu inaweza kujiendesha na kupata
faida bila kutoa au kupokea riba. Kwa kweli ipo mikataba ya kiislamu ya
kibiashara ambayo benki ya kiislamu inaweza kuitumia katika kutengeneza bidhaa
na huduma zake za kibenki ambazo zitakua zina afikiana na shari’ah ya kiislamu.
Moja
ya kazi muhimu ya benki katika uchumi ni kuwa kiunganishi baina ya kundi lenye
akiba na kundi la wawekezaji. Benki hupokea fedha kutoka wa waeka akiba
(savers) na wawekezaji (investors) huwezeshwa na benki kwa kutumia fedha hizo
kuwekeza katika miradi mbalimbali. Kwa kazi hii benki hujulikana kama “Financial
intermediary”.
Benki
hufanya kazi hii kwa kutengeneza na kutoa bidhaa mbalimbali za kibenki kwa
kuzingatia hitajio la wateja wake.
Benki
ambazo si za kiislamu huwa kiungo baina ya waeka akiba na wawekezaji kwa
kutengeneza bidhaa za kibenki zenye kuhusisha riba. Benki hizo hupokea fedha
kwa wateja wake kisha huzitumia kuwakopesha wateja wake wengine ambapo hulipa
riba kubwa kuliko ile benki itakayo walipa wateja wake wenye fedha hizo. Tofauti
ya kiasi cha riba benki inachopokea katika kukopesha na ile inayowalipa
walioweka akiba huhesabika kama faida kwa benki hiyo.
Kwa
mfano benki huweza kuwalipa asilimia saba (7%) waeka akiba wanapoeka fedha zao
benki na benki kutumia fedha hizo kuwakopesha wawekezaji ambao inaweza kuwatoza
riba ya asilimia kumi na tano (15%), tofauti kati ya 15% na 7% ambayo ni 8%
huchukuliwa kama faida kwa benki.
Benki
ya kiislamu hufanya kazi hii si kwa misingi ya riba. Benki ya kiislamu kama
benki ya kibiashara ina bidhaa za kibenki ambazo huweza kugawanya katika
makundi matatu.
Kundi
la kwanza ni bidhaa za Amana (Deposit Products), kundi la pili ni bidhaa za
uwezeshaji (Financing Products) na kundi la tatu ni bidhaa zinazohusisha huduma ambazo benki hutoa kwa kutoza ada (Fee
based Products).
Kundi
la kwanza la bidhaa za Amana linajumuisha bidhaa mbalimbali ambazo benki
huzitumia kukusanya fedha kutoka kwa wateja wake. Kwa ujumla katika kundi hili
bidhaa hugawanyika tena katika makundi matatu ambayo ni akaunti ya hundi
(Current account), akaunti ya akiba (Saving account) na akaunti ya muda maalumu
(Fixed deposit account) au akaunti ya uwekezaji (Investment account).
No comments:
Post a Comment